UMAJARIBIO KATIKA TAMTHILIYA YA NGUZO MAMA

     UCHAMBUZI WA TAMTHILIYA 

JINA LA TAMTHILIYA;NGUZO  MAMA.

MWANDISHI :PENINA MHANDO.

MCHAPAJI:Dar  es salaam university press.

MWAKA:1982.

UTANGULIZI

Tangu  umoja wa mataifa kutangaza kuwa 1975 ni mwaka wa wanawake Duniani juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanywa kuwakomboa wanawake kutoka na ukandamizwaji na udhalilishaji.Swali la kujiuliza ni je? Juhudi hizo za kumkomboa mwanamke zimefanikiwa? Na kama zimefanikiwa ni kwa kiasi gani?

Nguzo mama ni tamthiliya inayochimbua matatizo yanayo wakabili wakina mama katika juhudi zao za kujikomboaa ambapo matatizo haya yamegawanyika katika Nyanja zote za maisha ya kiuchumi,kisiasa,kiutamaduni na kijamii.

A.MAUDHUI.

    Ni jumla ya mawazo yote  ambayo huwekwa bayana na mtunzi wa kazi za fasihi.Na huhusisha dhamira,ujumbe,funzo,falsafa na mtigogoro.

DHAMIRA

     Ni lengo au kusudio alilokusudia msanii wa kazi za fasihi kufikisha kwenye jamii au hadhira yake.Ambapo kunadhamira kuu na dhamira ndogondogo.Katika tamthilya ya Nguzo Mama msani amejadili dhamira mbalimbali ambapo dhamira kuu ni Ukombozi wa Mwanamke.

Dhamira Ndogondogo.

1.Suala la ulevi.

      Msani amejadili suala la ulevi kama kikwazo kikubwa cha maendeleo katika tamthiliya Nguzo mama kupitia wahusioka mbalimbalik kama vile Bwana sudi,Shaba na totoro ambao wanaonekana wanatumia muda mwingi katika unywaji wa pombe kuliko kazi.Mfano msani katika tamthiliya:-Bwana sudi anasema:-

    …Kelele! Sasa mimi nitavaa nini.utaikausha kwa moto hiyo   nakwambia.Mimi nataka kurudi nilikotoka nimeacha pombe kafiri… (Uk 35-37)

Hivyo msani ameonesha kuwa ulevi ni kikwazo cha maendeleo ya jamii na ukombozi wa wanawake.

2.Suala mfumo dume,

      Pia msani amejadili suala hili kuonyesha jinsi wanaume wanavyo wachia majuku wanawake hata majukumu ambayo wanapaswa kutimiza wanashindwa kuyatimiza huku wengi wao wakijikita katika ulevi.Katika tamthiliya msani amemtumia Bwana Sudi anashindwa  kummbembeleza motto akiamini  suala kulea watoto ni la wanawake mfano msanii anasema;-

Sauti:Mama!mama!mama! mtoto analia.

    Bi.pili: (upesi anaachia kamba na kukimbilia upande inakotokea   sauti) mwanangu huyu jamani.(anakutana na sudi kalewa)

   Sudi:ulikuwa wapi saa zote hizi.Mimi nimekuja zamani  hapa,mtoto analia tu,sijui wewe uko wapi. (Uk 37)

Hivyo basi msani anaonyesha jinsi gani mfumo dume unavyokwamisha maendeleo na ukombozi wa wanawake kwani Bi.pili anaachia kamba na kukimbia kumbembeleza mtoto hivyo basi jamii iachane na mfumo huu kandamizi.

3.Hali ngumu ya maisha

     Msani amesawili jamii kwa kujadili suala la hali ngumu ya maisha kama tatizo sugu ambalo halijapatiwa tiba.Kwa kuwatumia wahusika kadha wa kadha kama vile Bi.pili na Mumewe Sudi.Mfano msani anaonyesha kuwa Bwana Sudi anashati moja tu.Mfano anasema;-

     …Kelele! Sasa mimi nitavaa nini.utaikausha kwa moto hiyo nakwambia.Mimi nataka kurudi nilikotoka nimeacha pombe  kafiri… (Uk 35-37)

Msani anaitaka jamii kujishughulisha katika shughuliza za kiuchumii ili kuweza kuondokana na hali ngumu ya maisha.

4.Suala la dhuluma kwa wajane.

      Msani ameonyesha suala hili kama kikwazo  cha wanawake kujikomboa kiuchumi kwani baada ya kufiwa na waume zao wamekuwa wakinyanganywa mali zote ambazo anacha mumewe na kiuchukuliwa na ndugu wa mume wake(mashemeji).Mfano katika tamthiliya ya Nguzo mama amemtumia mhusika Bi.saba anayenyanganywa mali zote baada ya kufiwa na mume wake. Mfano Bi.saba anasea;-

    …Mmerudi kuchukua hata kitanda,hata sufuria nitapika wapi nitalala wapi mimi ?....

Hivyo msani anawataka wanajamii kupiga vita suala hili ili kuweza kuchochea maendeleo katika jamiii.

          2.UJUMBE

1.Ulevi ni chanzo cha migogoro katika jamii.

2.Suala la dhuluma kwa wajane ni kikwazo       cha maendeleo ya wamawake.

3.Mfumo dume ni kikwazo cha maendeleo        ya jamii.

4.Umoja ni fimbo ya mnyonge.

          3.MIGOGORO

1.Mgogoro kati ya Bi.nane na Bi,nne.

    Chanzo;Wivu wa Bi.nne dhidi ya Bi.nane.

2.Mgogoro Bw.Sudi na Bi.pili

    Chanzo;Ulevi na mfumo dume aliokuwa          nao Bwana Sudi.

3.Mgogoro wa Sudi dhidi ya Totoro naShaba. Chanzo:Shaba na Totoro kumtetea Bi.pili.

            4.MSIMAMO.

                  Msani anamsimamo wa kimapinduzi kwani anaamini matatizo yote yanayowakabili wanawake yataondoka endapo watakuwa na umoja na shikamano.



   2.FANI.

            Ni umbo la nje la kazi ya fasihi.Huhusisha muundo,mtindo,mandhari wahusika na Matumizi ya lugha.

           1.MUUNDO.

                Ni mpangilio wa visa na matukio katika kazi ya fasihi.ambapo tamthiliya ya Nguzo mama msani ametumia muundo wa moja kwa moja ambao anaonyesha harakati za kuiinua nguzo mama na change moto zinazowakabili wanawake na hatimaye wanashindwa kuiinua Nguzo mama.

           2.WAHUSIKA.

                Hawa ni viumbe ambao hutumiwa na wasanii kuwakilisha kile anacholenga kufikisha kwenye jamii husika na wahusika ndio hubeba matukio yote yanayopaswa kuwasilishwa katika jamii.Hivyo msanii ametumia wahusika mbalimbali kama ifuatavyo:-

1.Bwana Sudi.

      Mme wa Bi.pili.

      Mlevi

      Anashikilia mfumo dume..


2.Bi pili.

       Mke wa sudi.

       Ananyanyaswa na Mumewe.

        Anajishughulisha na uuzaji wa pombe.

3.Chizi

        Mfichua maovu.


       3.MTINDO.

             Ni namna ya uwasilishaji wa kazi ya fasihi unaomtofautisha mtunzi mmoja na mwingine na huhusika zaidi na kitu kinacho itwa Umajaribio.

                    UMAJARIBIO

                          Ni matumizi ya tanzu au vipengele vya fasihi simulizi katika kazi ya fasihi andishi aidha tamthiliya na riwaya.Kwa kutumia tamthiliya ya Nguzo Mama iliyo andikwa na Penina Mhando msani huyo ametumia umajaribio katika kazi yake kwan amechota vipengele vya fasihi simulizi na kuvitumia katika kufikisha ujumbe katika jamii aliyokusudia kama ifuatavyo;-

1.MATUMIZI YA NYIMBO.

Nyimbo kama tanzu za fasihi simulizi zimeweza kutumiwa na msanii katika kazi yake.Penina Mhando ametumia nyimbo kutoka katika fasihi simulizi ili kuweza kufikisha kile alichokusudi kwa jamii.Mfano amewatumia wahusika kama vile Shaba na Totoro ili kuonyesha dhamira ya ulevi ambapo anawaonyesha wakiimba wakisema

        Tia lijae,

        Hilo kimbo,

        Siyo nusu,

        Tia lijae.(Uk 14)

Hivyo basi msani kupitia wimbo huu ameonyesha suala la ulevi kama linavyojitokeza katika jamii ya sasa.

2.MATUMIZI YA HADITHI.

Pia msani katika tamthiliya hii ametumia hadithi katika kufikisha kile alichokusudia kwa jamii husika,Mfano amemtumia mhusika Bi.msimulizi ambaye anasema;-

      Bi.msimulizi:Hadithi! Hadithi!

      Hadhiara:Hadithi njoo!

      Bi.msimulizi:Hadithi! Hadithi!

      Hadhiara:Hadithi njoo! (Uk 3-4)

Hivyo kupitia hadithi msani ameweza kufichua maovu na changamoto zote zinazo wakabili wanawake katika juhudi za kijikomboa.

3.MATUMIZI YA NGOMA.

Pia msani ametumia ngoma  ambao ni utanzu wa fasihi simulizi katika kazi yake ili kuweza kuvutta umakini wa hadhira yake na kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jami yake.Mfano ametumia ngoma pale mtangazaji anaokua anatangaza ambapo anasema:-

   ….la mgambo likilia lina jambo(ngoma anaondo) (uk 45)

Hivyo msani ametumia ngoma kuipa kazi yake mvuto ili isimchoshe hadhira  anayesoma kazi hii. 

4.MATUMIZI YA SEMI.

   Pia msani ametumia semi mbalimbali katika kazi yake  kama vile methali,Nahau na misemo ili kuweza kusawili vema jamii yake.Mfano msanii ametumia nahau pindi mtangazaji anaokuwa akitangaza akisema;-

  ….la mgambo likikilia lina jambo….uk 45

….utakiona cha mtema kuni..

Hiyo yote inamampa msani uwezo wa kuweza kueleza masuala jinsi ytyalivyo katika jamii na kuweza kuipa kazi yake mvuto wa kipekee.

  Maswali ya kujiuliza.

1.Je kuna umuhimu wa vipengele vya fasihi simulizi katika tamthiliya?

2.Kama ni ndio umuhimu huo ni upi?


Imeandaliwa na Sir. Dyampaye na Arosius M Kabaija

 

Toa maoni yako kwa hii kazi ili tujifunze zaidi na kuboresha huduma hii ya solving za  maswali mbalimbali.

     TOA MAONI YAKO HAPO CHINI 

ILI KUFANYA MABORESHO PIA HAKIKISHA UMEFOLLOW BLOG HII FOR MORE SOLVINGS 



Picha yake Kwa juu Ndo hiyo hapo Kwa wale WANAOHITAJI kuijua.



Next Post Previous Post
8 Comments
  • Dyampaye
    Dyampaye 31 يناير 2023 في 10:05 ص

    JAMANI TOENI MAONI YENU HAPA TUJUE MABORESHO TUNAYAFANYA WAPI..

    • غير معرف
      غير معرف 17 فبراير 2023 في 12:00 ص

      Kazi nzuri

  • غير معرف
    غير معرف 31 يناير 2023 في 11:52 ص

    Kazi ipo good

    • Dyampaye
      Dyampaye 31 يناير 2023 في 12:50 م

      Pamoja sanaa

  • غير معرف
    غير معرف 1 فبراير 2023 في 2:24 ص

    Matumizi ya lugha

    • Dyampaye
      Dyampaye 1 فبراير 2023 في 3:28 ص

      Usiwaze coming soon..

  • غير معرف
    غير معرف 1 فبراير 2023 في 11:47 م

    Untama

  • غير معرف
    غير معرف 3 فبراير 2023 في 10:52 ص

    Iko vizur sana nyongeza ni ushauri tu kwa watu wazid kushare na kucoment link hii kwa wanafasihi mbalimbali

Add Comment
comment url