UMAJARIBIO KATIKA TAMTHILIYA YA MZALENDO KIMATHI

       UMAJARIBIO KATIKA TAMTHILIYA

TAMTHILIYA:MZALENDO KIMATHI.

MWANDISHI:NGUNGI WA THIONG’O.

PUBLISHER: East African Educational Publishers.

Mwaka:1978.

Utangulizi

Tamthiliya ya Mzalendo Kimathi iliandikwa na Ngungi Wa Thiong’o mnamo mwaka 1976 na kilitolewa kwa Kiswahili na East African educational publisher mnamo mwaka 1978.

Tamthiliya hii inahusu harakati za kudai uhuru nchini Kenya  ambapo tunaona wananchi wa Kenya wanapigana vita vya Maumau dhidi ya ukoloni wa Mwingereza na katika harakati hizo wanakumbana na changamoto mbalimbali kama vile viongozi wao kufungwa jela na wakoloni.

Tamthiliya ya MZALENDO KIMATHI


                  UMAJARIBIO

Waandishi wa Tamthiliya ya Mzalendo Kimathi wametumia mbinu mbalimbali za fasihi simulizi katika kuwasilisha yale waliyokusudia katika jamii husika.Na mbinu hizo ni kama ifuatavyo;-


1.Matumizi ya Nyimbo.

   Katika onyesho la kwanza waandishi wameonyesha wananchi wakiimba nyimbo zinazodhirisha  mapambano dhidi ya ukoloni au watu weupe waliokuwa wakitawala kwa mabavu na manyanyaso.Mfano katika ukurasa wa Kwanza (uk 1) wananchi wanaimba kama ifuatvyo:-

            Tutanyakua mashamba yetu,

            Tupiganie uhuru wetu,

            Tuikomboe elimu yetu,

             Tutanyakua viwanda vyetu….

Wimbo huu umetumika kutoa hamasa na kuonyesha nia ya wananchi wa Kenya dhidi ya kupambana na ukoloni na kupigania uhuru wao.


2.Matumizi ya Ngoma.

   Pia katika Tamthiliya hii waandishi wametumia ngoma kama kipera moja wapo cha fasihi simulizi katika kufikisha ujumbe na kuvuta umakini wa hadhira katika kuisoma kazi hii ya fasihi. Mfano katika onyesho la Kwanza (uk 1).Ambapo anasema:-

      …Midundo ya ngoma inasikika kwa Mbali lakini inaendelea kuwa na sauti kubwa mpaka mwisho hkuna sauti nyingine isipokuwa midundo….

Hivyo basi  msanii ametumia Ngoma katika kazi yake ili kuvuta umakini wa hadhira na kumhamasisha hadhira kendele kusoma kazi hiyo.


3.Matumizi ya Takiriri.

   Ni tamathali ya semi ambapo neno hurudiwa zaidi ya mara moja.Katika tamthiliya ya Mzalendo Kimathi msanii ametumia mbinu hii kama njia ya kuweka msisitizoau kusisistiz jambo fuani analotaka kuwasilisha kwa jamii aliyokusudia.Mfano ametumia takiriri katika kurasa mbalimbali Mfano katika (uk 23) anasema ;-

     -Sheria ni sharia.

     -Haki ni haki.  

Pia katika ukurasa wa 35 Kimathi anasema;-

    Maendeleo!Pesa.Pesa ni maendeleo?

Hivyo msani ametumia takiriri ambayo ni mbinu ya fasihi simulizi katika fasihi andishi kwa nia ya kuweka msisitizojuuu ya kuile alichokusudia kufikisha kwa hadhira iliyokusudiwa.


4.Matumizi ya Vicheko.

   Katika tamthiliya ya Mzalendo Kimathimsanii ametumia vicheko ili kuiipamba kazi yake na kuipa Mvuto kwa wasomaji wake.Mfano katika ukurasa wa 36 (uk 36) Mwenye benki anacheka kama;

     Ha! Ha! Ha! U mtu mwenye busara Dedan la.Hakuna haja ya  Kupigana na mabenki…

Hivyo ametumia kicheko kama njia ya kuipamba kazi yake ili iweze kumvutia hadhira kuendelea kuisoma bila kuchoaka.


JINA LA TAMTHILIYA;NGUZO  MAMA.

MWANDISHI :PENINA MHANDO.

MCHAPAJI:Dar  es salaam university press.

MWAKA:1982.

1.MATUMIZI YA NYIMBO.

Nyimbo kama tanzu za fasihi simulizi zimeweza kutumiwa na msanii katika kazi yake.Penina Mhando ametumia nyimbo kutoka katika fasihi simulizi ili kuweza kufikisha kile alichokusudi kwa jamii.Mfano amewatumia wahusika kama vile Shaba na Totoro ili kuonyesha dhamira ya ulevi ambapo anawaonyesha wakiimba wakisema

        Tia lijae,

        Hilo kimbo,

        Siyo nusu,

        Tia lijae.(Uk 14)

Hivyo basi msani kupitia wimbo huu ameonyesha suala la ulevi kama linavyojitokeza katika jamii ya sasa.


2.MATUMIZI YA HADITHI.

Pia msani katika tamthiliya hii ametumia hadithi katika kufikisha kile alichokusudia kwa jamii husika,Mfano amemtumia mhusika Bi.msimulizi ambaye anasema;-

      Bi.msimulizi:Hadithi! Hadithi!

      Hadhiara:Hadithi njoo!

      Bi.msimulizi:Hadithi! Hadithi!

      Hadhiara:Hadithi njoo! (Uk 3-4)

Hivyo kupitia hadithi msani ameweza kufichua maovu na changamoto zote zinazo wakabili wanawake katika juhudi za kijikomboa.

     

3.MATUMIZI YA NGOMA.

Pia msani ametumia ngoma  ambao ni utanzu wa fasihi simulizi katika kazi yake ili kuweza kuvutta umakini wa hadhira yake na kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jami yake.Mfano ametumia ngoma pale mtangazaji anaokua anatangaza ambapo anasema:-

   ….la mgambo likilia lina jambo(ngoma anaondo) (uk 45)

Hivyo msani ametumia ngoma kuipa kazi yake mvuto ili isimchoshe hadhira  anayesoma kazi hii. 


4.MATUMIZI YA SEMI.

   Pia msani ametumia semi mbalimbali katika kazi yake  kama vile methali,Nahau na misemo ili kuweza kusawili vema jamii yake.Mfano msanii ametumia nahau pindi mtangazaji anaokuwa akitangaza akisema;-

  ….la mgambo likikilia lina jambo….uk 45

  ….utakiona cha mtema kuni..

Hiyo yote inamampa msani uwezo wa kuweza kueleza masuala jinsi ytyalivyo katika jamii na kuweza kuipa kazi yake mvuto wa kipekee.


  Maswali ya kujiuliza.

1.Je kuna umuhimu wa vipengele vya fasihi simulizi katika tamthiliya?

2.Kama ni ndio umuhimu huo ni upi?


Prepared By Sir Dyampaye and Sir Gresmo

To get pdf please call us 0766201936/0694179206

      Click Download to get Pdf soft copy

                     DOWNLOAD PDF


Please Tunaomba SAPOTI Yako bonyeza Video hiyo Hapo Kisha Subscribe Share and comments Ili KUENDELEA na kazi 


Please nakuomba Subscribe Kwa Channel hiyo ya YouTube Kupeana Moyo na SAPOTI KUENDELEA na Kazi ya taaluma



Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url