PRAGMATIKI FULL HAND OUT
PRAGMATIKI
Masamba 2004;anasema pragmatiki ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa lugha katika mawasiliano.
Kahili 2019;anasema pragmatiki ina lengo la umilisi wa kipragmatiki wa maana ya lugha.
UMILISI WA KIPRAGMATIKI
Ni uwezo wa kuelewa maana ya lugha kutokana namuktadha uliopo.Maana ya kipragmatiki hufungamana na muktadha.
Kwa ujumla;Pragmatiki ni taaluma ya isimu inayohusika na kuchunguza jinsi muktadha unavyoasili maana.Pia pragmatiki inafafanua matumizi ya lugha ya watu katika Miktadha mbalimbali.
MUKTADHA;Ni mjumuiko wa mambo mbalimbali.Mambo hayo ni kama yafuatayo:-
1.Anamzungumzia nani?(Msikilizaji)
2.Wanazungumza wakiwa wapi(Eneo)
3.Unazungumza na kundi gani?
4.Wanazungumzia nini? (Mada)
5.Ni wakati gani?(Wakati/Muda)
6.Wana lengo gani?(Dhamira)
7.Mtazamo wao ni upi?
8.Wapo katika hali gani?
-Huzuni,Furaha au ucheshi n.k
DHANA KATIKA PRAGMATIKI
1.VIMANILIZI
Ni maana inayoibuliwa kutokana na kile kinachosemwa.
Mfano,Nina hisi baridi kimanilizi chake ni kuzima feni kama imewashwa.
Mbu wanaingia kimanilizi chake ni kufungamlango.
2.UDHAMILIZI
Ni maana inayotambuliwa katika muktadha ambapomsemaji hudhani kuwa msikilizaji anatarifa za awali juu ya kile kisemwacho sasa.
Mfano,Mtoto wa Juma anaumwa ambapo udhamilizi wake ni Juma kuwa na mtoto/Juma ana mtoto.
3.MATENDO UNENI
Ni matendo yanayotendwa kupitia uneni(Kunena).
Mfano,Nina kuhukumu miaka tisa jela.
Nina ahidi kukupenda maisha yangu yote.
UHUSIANO WA PRAGMATIKI NA
SEMANTIKI.
1.Matawi yote mawili yanajikita katika kuchunguza maana katika lugha.
-Ili maana za kipragmatiki ziweze kuchunguzwa ni lazima tungo iwe na maana kisemantiki.
2.Uelewakaji wa maana za ziada zinazofafanuliwa katika taaluma ya semantiki huhitaji Muktadha.
UTOFAUTI WA PRAGMATIKI NA
SEMANTIKI.
1.Maana.
2.Lengo.
3.Vipengele vinavyochunguzwa.
Mwisho
Toa maoni yako sehemu ya coment maboresho yafanyike
kama unaswali uliza pia your free.......
Please follow our blog