SEMANTIKI NA PRAGMATIKI FULL HAND OUT

              

                            HAND OUT 
               SEMANTIKI NA PRAGMATIKI.
Semantiki;ni tawi linalojishighulisha na uchunguzi wa maana katika lugha ya mwanadamu.Huanza kuchunguza katika kiwango cha sauti,Mofimu,Neno hadi tungo.
           

                

           MALENGO YA SEMANTIKI
1.Hushughulika na mpangilio wa sauti unaoleta maana katika neno.
2.Hushughulika na uainishaji wa maana za maneno.
3.Hushughulika na maana za tungo.
4.Hushughulika na taratibu zote za kuchambua maana.
5.Hushughulika na asili ya neno.
6.Huhusika na nadharia za uchambuzi wa maana.

                      MAANA
Nini maana ya maana ?
Hakuna fasili kamili ya neno maana wala Maanisha.Watu  wa mwanzo 1923 wanadai kuwa maana ya Maana ni tete.
Hivyo kuna mitazamo mbalimbali ambayo imeelezewa  na watalaamu mbalimbali kuelezea maana ya Maana.
   
     MITAZAMO INAYOELEZEA MAANA YA  MAANA

1.MAANA KAMA KITAJWA.
   Hulejelea umbo fulani la kiisimu.Na mtazamo huu umeasisiwa na Fodor 1980 Pamoja na Akmojian na Wenzake 2010. Ambapo wanasema umbo lolote kama linamaana lina maana lazima liwe na kirejelewa.Majina/Nomino ndiyo huwa na umbo.

                      UBORA
1.Kuna ukweli katika lugha kuna maneno yanapata maana kwa  
   kurejelea  umbo.
2.Watoto hujifunza  lugha kwa kuonyeshwa vitu.

                       UDHAIFU 
1.Kunamaneno yasiyotaja vitu halisi.Mfano hapana
2.Maumbo tofauti tofauti huweza kurejelea kitu kimoja lakini   
    yanakuwa na maana tofauti.Mfano Fedha,Pesa na hela.
3.Majina ya dhahania yanakosa maana.Mfano njaa, upepo n.k

2.MAANA KAMA DHANA YA MSINGI
    Mtazamo huu umeasisiwa na  Palmer 1976 na Lyons 1987.Ambapo wanasema Maana ni ile fikira au wazo lililoko akilini mwa mtu.
        
                      UBORA 
1.Maneno dhahania huweza kupata maana.
2.Huonyesha maana za maneno hutokana na dhana.

                     UDHAIFU
1.Kuna maneno hayana dhana wala taswira hivyo yanakosa maana kwani mawazo ya Mtu hayatoshi   
   kuelezea maana ya kitu

3.MAANA KAMA  MWITIKO.
   Mtazamo huu umeasisiwa na  Broomfield 1933.Ambapo anasema Maana ni mwitiko wa msikilizaji.Kwani kila mtu anaposikia neno au sentensi huibua hisia na mtazamo wake akilini mwake.
  
                   UDHAIFU
1.Tafsiri zote mbaya za maneno ni kulingana na alivyoitikia.

                    UPUNGUFU
1.Si kila wakati watu wana mwitiko sawa juu  ya kitu.
2.Kuna maneno hayana mwitiko  wa wazi.Mfano viunganishi.

4.MAANA KAMA MATUMIZI 
    Mtazamo huuumeasisiwa na Wittgenstein 1953.ambapo anasema maana isiwekewe mipaka,ni kosa  kubwa  badala yake tuzingatie matumizi ya umbo hilo.
-Maana ya tamko hupatikana katika atumizi yake.
-Hivyo maana huakisi utamaduni fulani wa jamii vilevile huendana na taratibu zote za matumizi ya lugha kama:-
 Muktadha,Wahusika, na Wakati n.k

                   UBORA
1.Hufanya maana za maneno kuwa wazi bila uvuli vuli.
2.Maneno yote huwa na maana hatakama hayana virejelewa .Mfano lakini,ila n.k
3.Huweza kutofautisha maneno yenye maana zaidi ya moja.

                   UPUNGUFU  
1.Hauweki mipaka ya kimatumizi aidha katika jamii au sentensi.
2.Kuna maneno ambayo yanaweza kupata maana hata  
   kabla ya kutumika.Mfano Jua,Aridhi n.k 
3.Maneno hayana maana kwa upekee wake.

                  AINA ZA MAANA
1.MAANA MSINGI.
   Hii ni maana ya kimantiki yani fasili ya wazi ya neno.Yani fasili ya wazi ya neno.Ni fasili ya umbo la kiisimu(neno).
      
                     KANUNI ZAKE.
1.Muundo wa vijenzi maana
2.Muundo wa vijenzi maana kinzani.

                     AMBAPO 
kijenzi maana;-Ni kile kinacotoa maana tafsiri kamili ya maana ya neno.
 Kijenzi kinzani;-ndicho ambacho hututofautishia maana.
            Mfano, Mwanaume
                             +Mtu mzima.
                             +Jinsia ya kiume.

2.MAANA ZIADA.
     Ni fasili ya umbo la kiisimu ambayo inategemea  muktadha au hisia za mzungumzaji.
-Maana hutofautiana kutegemeana na mtazamo wa watu,kikundi  au jamii.
-Pia hurejelea maana ya msingi.
Mfano;-Mzee-Mtu mzima kuanzia miaka 45+
                      -Ni mtu mwenye fedha nyingi.
                      -Kupata cheo/Neno la heshima kazini.
Pia maana hizi hutofautiana kutokana na mazingira ya kijamii na kipindi fulani cha wakati wa kihistoria.
NB.Sio sehemu muhimu ya lugha mpaka itakapo sanifishwa.

3.MAANA YA HISIFU.
      Maana hutoka na hisia binafsi za msemaji pamoja na tabia yake kwa msikilizaji wake.Pia hutegemea mwonekano wake juu ya kile anachokizungumza.
-Hisi innategemeana na kiimbo
-Pia hutegemeana na kidatu.
-Hutegemea pia sauti.
Mfano lugha ya majivuno katika kueleza.Jembe,Mwamba n.k

4.MAANA AKISI/PICHA/TASWIRA.
   Dhana moja ya neno inaksi picha au taswira mbalimbali pia dhana ya neno pia inakisi sehemu ya mwitiko kwa dhana nyingine.
Mfano;-Chakachua
             Naenda uwani.
Pia tafsida huingia katika kundi hili la maana  akisi.

NOTE:TOA MAONI YAKO HAPO CHINI SEHEMU YA COMMENT FOR MORE IMPROVEMENT PLEASE SAPOTI YAKO NI MUHIMU SANA 

                    TOA SAPOTI YAKO 

Jamani NAOMBA SAPOTI YAKO SUBCRIBE
Jinsi Bwana HARUSI ALIVYO LIZA WATU 
Kwa wimbo wake kwenye sherehe.

                    DOWNLOAD

Next Post Previous Post
1 Comments
  • Anonymous
    Anonymous February 11, 2023 at 11:54 PM

    yusralemah904@gmail.com

Add Comment
comment url